Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 11 - يسٓ - Page - Juz 22
﴿إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكۡرَ وَخَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِۖ فَبَشِّرۡهُ بِمَغۡفِرَةٖ وَأَجۡرٖ كَرِيمٍ ﴾
[يسٓ: 11]
﴿إنما تنذر من اتبع الذكر وخشي الرحمن بالغيب فبشره بمغفرة وأجر كريم﴾ [يسٓ: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika ni kwamba uonyaji wako unamfaa mwenye kuiamini Qur’ani, akafuata hukumu za Mwenyezi Mungu zilizo ndani yake na akamuogopa Mwingi wa rehema akiwa mahali ambapo hakuna amuonaye isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi huyo mpe bishara njema ya kuwa atapata msamaha wa dhambi zake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na atapata malipo mema kutoka Kwake huko Akhera kwa matendo yake mema, nayo ni Pepo |