Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 38 - يسٓ - Page - Juz 23
﴿وَٱلشَّمۡسُ تَجۡرِي لِمُسۡتَقَرّٖ لَّهَاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ ﴾
[يسٓ: 38]
﴿والشمس تجري لمستقر لها ذلك تقدير العزيز العليم﴾ [يسٓ: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na alama kwao (ya utendakazi wa Mwenyezi Mungu) ni jua ambalo linatembea hadi kituo chake Alichokikadiria Mwenyezi Mungu, halitakipita kituo hiko wala halitatulia kabla ya kukifikia. Huo ni mpango wa Mshindi Asiyeshindwa, Mjuzi Ambaye hakuna kitu chochote kinachofichamana na ujuzi Wake |