Quran with Swahili translation - Surah sad ayat 8 - صٓ - Page - Juz 23
﴿أَءُنزِلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ مِنۢ بَيۡنِنَاۚ بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ مِّن ذِكۡرِيۚ بَل لَّمَّا يَذُوقُواْ عَذَابِ ﴾
[صٓ: 8]
﴿أؤنـزل عليه الذكر من بيننا بل هم في شك من ذكري بل﴾ [صٓ: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Je, amehusishwa Muhammad peke yake kwa kuteremshiwa Qur’ani bila ya sisi?» Bali wao wako kwenye shaka ya kuwa mimi nimekuletea wahyi wewe, ewe Mtume, na kukupa utume. Bali wao walisema hilo kwa kuwa hawajaonja adhabu ya Mwenyezi Mungu, na lau wangaliionja adhabu hawangalithubutu kusema waliyosema |