×

Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao 39:10 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Az-Zumar ⮕ (39:10) ayat 10 in Swahili

39:10 Surah Az-Zumar ayat 10 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 10 - الزُّمَر - Page - Juz 23

﴿قُلۡ يَٰعِبَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡۚ لِلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۗ وَأَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٌۗ إِنَّمَا يُوَفَّى ٱلصَّٰبِرُونَ أَجۡرَهُم بِغَيۡرِ حِسَابٖ ﴾
[الزُّمَر: 10]

Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل ياعباد الذين آمنوا اتقوا ربكم للذين أحسنوا في هذه الدنيا حسنة, باللغة السواحيلية

﴿قل ياعباد الذين آمنوا اتقوا ربكم للذين أحسنوا في هذه الدنيا حسنة﴾ [الزُّمَر: 10]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Sema, ewe Nabii, kuwaambia waja wangu wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, «Mcheni Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kujiepusha na matendo ya kumuasi.» Na wale waliofanya wema katika dunia hii kwa kumuabudu Mola wao na kumtii watapata wema huko Akhera, nao ni pepo, na wema huko duniani, ambao ni afya, riziki, ushindi na vinginevyo. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu, basi hamieni humo muende pale ambapo mtamuabudu Mola wenu na mtamakinika kusimamisha Dini yenu. Hakika Mwenyezi Mungu Atawapa wenye kuvumilia malipo yao mema huko Akhera bila mpaka wala hesabu wala kipimo. Huku ni kuyafanya makubwa malipo ya wenye kusubiri na thawabu zao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek