Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 9 - الزُّمَر - Page - Juz 23
﴿أَمَّنۡ هُوَ قَٰنِتٌ ءَانَآءَ ٱلَّيۡلِ سَاجِدٗا وَقَآئِمٗا يَحۡذَرُ ٱلۡأٓخِرَةَ وَيَرۡجُواْ رَحۡمَةَ رَبِّهِۦۗ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُونَ وَٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ ﴾
[الزُّمَر: 9]
﴿أمن هو قانت آناء الليل ساجدا وقائما يحذر الآخرة ويرجو رحمة ربه﴾ [الزُّمَر: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, kafiri huyu anayejistarehesha na ukafiri wake ni bora au ni yule anayemuabudu Mola wake na kumnyenyekea, anatumia nyakati za usiku kusimama kwenye Ibada na kumsujudia, anaogopa adhabu ya Akhera na kutarajia rehema ya Mola wake? Sema, ewe Nabii, «Je, wanalingana wale wanaomjua Mola wao na dini yao ya haki na wale wasiojua chochote katika hayo?» Hawalingani. Kwa hakika wanaokumbuka na kujua tafauti ni wale wenye akili timamu |