×

Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanao wafanya 39:3 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Az-Zumar ⮕ (39:3) ayat 3 in Swahili

39:3 Surah Az-Zumar ayat 3 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 3 - الزُّمَر - Page - Juz 23

﴿أَلَا لِلَّهِ ٱلدِّينُ ٱلۡخَالِصُۚ وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ مَا نَعۡبُدُهُمۡ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَآ إِلَى ٱللَّهِ زُلۡفَىٰٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ فِي مَا هُمۡ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَنۡ هُوَ كَٰذِبٞ كَفَّارٞ ﴾
[الزُّمَر: 3]

Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanao wafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu - Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayo khitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo kafiri

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألا لله الدين الخالص والذين اتخذوا من دونه أولياء ما نعبدهم إلا, باللغة السواحيلية

﴿ألا لله الدين الخالص والذين اتخذوا من دونه أولياء ما نعبدهم إلا﴾ [الزُّمَر: 3]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Jua utanabahi kwamba ni haki ya Mwenyezi Mungu, Peke Yake, kutiiwa utiifu uliyotimia uliosalimika na ushirikina. Na wale wanaomshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu wakawafanya wasiokuwa Yeye kuwa ni wategemewa, wanasema, «Hatuwaabudu waungu hawa pamoja na Mwenyezi Mungu isipokuwa wapate kutuombea kwa Mwenyezi Mungu na ili watukurubishe daraja Kwake.» Hivyo basi wakakufuru, kwani ibada na uombezi ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Atawapambanua, Siku ya Kiyama, baina ya Waumini wenye ikhlasi na wale wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, katika yale waliokuwa wanatafautiana juu yake kuhusu vile walivyoabudu. Hapo amlipe kila mmoja kwa anachostahiki. Hakika Mwenyezi Mungu hawaelekezi kuongoka kwenye njia iliyonyoka wale wenye kumzulia urongo Mwenyezi Mungu, wenye kuzikanusha aya Zake na hoja Zake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek