Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 42 - الزُّمَر - Page - Juz 24
﴿ٱللَّهُ يَتَوَفَّى ٱلۡأَنفُسَ حِينَ مَوۡتِهَا وَٱلَّتِي لَمۡ تَمُتۡ فِي مَنَامِهَاۖ فَيُمۡسِكُ ٱلَّتِي قَضَىٰ عَلَيۡهَا ٱلۡمَوۡتَ وَيُرۡسِلُ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ ﴾
[الزُّمَر: 42]
﴿الله يتوفى الأنفس حين موتها والتي لم تمت في منامها فيمسك التي﴾ [الزُّمَر: 42]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ndiye Anayezikamata nafsi wakati zinapokufa. Kufa huku ni kufa kukubwa, kufa kwa kushukiwa na mauti kwa ajali kukoma. Na zile nafsi ambazo hazikufa Anazikamata katika hali ya kulala kwake, nako ndiko kufa kudogo. Hivyo basi Akazizuia, kati ya hizi nafsi mbili, ile Aliyoitolea uamuzi ife , nayo ni ya yule aliyekufa, na anaiachilia nafsi nyingine mpaka ikamilishe muda wake wa kuishi na riziki yake, nako ni kuirudisha kwenye mwili wa mwenye nafsi hiyo. Kwa kweli, katika kule kukamata kwa Mwenyezi Mungu nafsi ya aliyekufa na aliyelala na kuiachilia nafsi ya aliyelala na kuizuia nafsi ya aliyekufa kuna dalili waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu kwa anayefikiria na kuzingatia |