Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 43 - الزُّمَر - Page - Juz 24
﴿أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُفَعَآءَۚ قُلۡ أَوَلَوۡ كَانُواْ لَا يَمۡلِكُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَعۡقِلُونَ ﴾
[الزُّمَر: 43]
﴿أم اتخذوا من دون الله شفعاء قل أو لو كانوا لا يملكون﴾ [الزُّمَر: 43]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Au kwani hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu wamewachukua badala Yake Yeye waungu wao wanaowaabudu wakawafanya ni waombezi wakuwaombea kwa Mwenyezi Mungu katika haja zao? Waambie, «Je mnawafanya ni waombezi kama mnavyodai, ingawa waungu hao hawamiliki chochote na hawafahamu kamwe kuwa nyinyi mnawaabudu |