Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 51 - الزُّمَر - Page - Juz 24
﴿فَأَصَابَهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُواْۚ وَٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡ هَٰٓؤُلَآءِ سَيُصِيبُهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُواْ وَمَا هُم بِمُعۡجِزِينَ ﴾
[الزُّمَر: 51]
﴿فأصابهم سيئات ما كسبوا والذين ظلموا من هؤلاء سيصيبهم سيئات ما كسبوا﴾ [الزُّمَر: 51]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yakawapata wale waliyosema kauli hii, miongoni mwa ummah waliopita, mateso ya matendo mabaya waliyoyachuma, hivyo basi wakaharakishiwa laana katika maisha ya duniani. Na wale waliojidhulumu nafsi zao katika watu wako, ewe Mtume, na wakasema kauli hii, yatawapata mateso ya yale mabaya waliyoyachuma kama yaliyowapata waliokuwa kabla yao, na hawakuwa wao ni wenye kumponyoka Mwenyezi Mungu wala kumshinda |