Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 159 - النِّسَاء - Page - Juz 6
﴿وَإِن مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ إِلَّا لَيُؤۡمِنَنَّ بِهِۦ قَبۡلَ مَوۡتِهِۦۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ شَهِيدٗا ﴾
[النِّسَاء: 159]
﴿وإن من أهل الكتاب إلا ليؤمنن به قبل موته ويوم القيامة يكون﴾ [النِّسَاء: 159]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kwa hakika hatasalia yoyote, kati ya wale waliopewa Kitabu, baada ya kuteremka ‘Īsā zama za mwisho, isipokuwa atamuamini Nabii ‘Īsā kabla ya kufa kwake, amani imshukie, na siku ya Kiyama Nabii ‘Īsā atakuwa ni shahidi kwamba waliomkanusha walikuwa warongo na waliomuamini walikuwa wakweli |