Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 54 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿أَمۡ يَحۡسُدُونَ ٱلنَّاسَ عَلَىٰ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۖ فَقَدۡ ءَاتَيۡنَآ ءَالَ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَءَاتَيۡنَٰهُم مُّلۡكًا عَظِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 54]
﴿أم يحسدون الناس على ما آتاهم الله من فضله فقد آتينا آل﴾ [النِّسَاء: 54]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Au je, kwani wao wanamhusudu Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye kwa neema za unabii na utume alizopewa na Mwenyezi Mungu na kuwahusudu Masahaba wake kwa neema ya kuongozwa kwenye Imani, kuukubali utume, kumfuata Mtume na kupewa uwezo katika ardhi, wakawa wanatamani neema hizi ziwaondokee? Hakika sisi tuliwapa watu wa kizazi cha Ibrāhīm, amani imshukiye, Vitabu Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwao, wahyi mwingine usiokuwa kitabu chenye kusomwa na tukawapa , pamoja na hayo, utawala wenye kuenea |