Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 60 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا ﴾
[النِّسَاء: 60]
﴿ألم تر إلى الذين يزعمون أنهم آمنوا بما أنـزل إليك وما أنـزل﴾ [النِّسَاء: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hukujua, ewe Mtume, mambo ya wale wanafiki wenye kudai kuwa wameyaamini yale uliyoteremshiwa, nayo ni Qur’ani, na yale waliyoteremshiwa Mitume kabla yako, ilhali wao wanataka kuhukumiwa, katika ugomvi unaotokea baina yao, kwa sheria ya batili, isiyowekwa na Mwenyezi Mungu, na wao waliamrishwa kuikataa batili? Shetani anataka kuwaepusha na njia ya haki na kuwaweka mbali nayo kabisa. Katika aya hii kuna dalili kwamba Imani ya kweli inalazimu kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu na kuitumia katika kutoa uamuzi juu ya kila jambo. Kwa hivyo, mwenye kudai kuwa ni Muumini na akachagua uamuzi wa Shetani juu ya uamuzi wa Mwenyezi Mungu, huwa ni Mrongo katika madai yake |