Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 31 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿مِثۡلَ دَأۡبِ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۚ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلۡمٗا لِّلۡعِبَادِ ﴾
[غَافِر: 31]
﴿مثل دأب قوم نوح وعاد وثمود والذين من بعدهم وما الله يريد﴾ [غَافِر: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Mfano wa mwenendo wa watu wa Nūḥ, 'Ād, Thamūd na waliokuja baada yao katika ukafiri na ukanushaji, ambao Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa sababu ya hilo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Hataki kuwafanyia maonevu waja, Akawa Atawaadhibu bila dhambi walilolitenda. Mwenyezi Mungu Yuko juu sana mno kwa kujiepusha na maonevu na upungufu |