Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 35 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡۖ كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلۡبِ مُتَكَبِّرٖ جَبَّارٖ ﴾
[غَافِر: 35]
﴿الذين يجادلون في آيات الله بغير سلطان أتاهم كبر مقتا عند الله﴾ [غَافِر: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Wale wanaobishana na aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake kwa kuzipinga bila kuwa na hoja zenye kukubalika, upinzani wao huo unawaletea machukivu makubwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa wale walioamini, kama Alivyopiga muhuri kwenye nyoyo za hawa wapinzani na Akazifinika zisiongoke, ndivyo Anavyoupiga muhuri moyo wa kila mwenye kiburi cha kumfanya akatae kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, aliye mjeuri sana kwa wingi wa udhalimu wake na uadui wake.» |