Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 34 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿وَلَقَدۡ جَآءَكُمۡ يُوسُفُ مِن قَبۡلُ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا زِلۡتُمۡ فِي شَكّٖ مِّمَّا جَآءَكُم بِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَا هَلَكَ قُلۡتُمۡ لَن يَبۡعَثَ ٱللَّهُ مِنۢ بَعۡدِهِۦ رَسُولٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَنۡ هُوَ مُسۡرِفٞ مُّرۡتَابٌ ﴾
[غَافِر: 34]
﴿ولقد جاءكم يوسف من قبل بالبينات فما زلتم في شك مما جاءكم﴾ [غَافِر: 34]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na Mwenyezi Mungu Aliwatumilizia kwenu Nabii mtukufu, Yūsuf mwana wa Ya’qūb, amani ziwashukie, kabla ya Mtume Mūsā, Akampatia dalili zilizo wazi juu ya ukweli wake, na Akawaamuru nyinyi kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake Asiye na mshirika, mkaendelea kuwa na shaka juu ya yale aliyokuja nayo katika kipindi cha uhai wake mpaka alipokufa. Na alipokufa shaka yenu iliongezeka na pia ushirikina wenu na mkasema, ‘Mwenyezi Mungu Hatatuma mjumbe baada yake.’ Mfano wa upotevu huu ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyompoteza kila anayeikiuka haki, mwenye shaka juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Asimuafikie kwenye uongofu na unyofu |