Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 56 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡ إِن فِي صُدُورِهِمۡ إِلَّا كِبۡرٞ مَّا هُم بِبَٰلِغِيهِۚ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ ﴾
[غَافِر: 56]
﴿إن الذين يجادلون في آيات الله بغير سلطان أتاهم إن في صدورهم﴾ [غَافِر: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika ya wale wanaoipinga haki kwa ubatilifu, na wanaozirudisha hoja sahihi kwa udanganyifu wa uharibifu bila ya kuwa na dalili wala ushahidi wala hoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hamna ndani ya nyoyo za hao isipokuwa kuifanyia kiburi haki, kwa uhasidi wao juu ya fadhila ambazo Mwenyezi Mungu Amempa mtume Wake na utukufu wa utume ambao Amemkirimu nao, nayo ni mambo wao si wenye kuyafikia wala kuyapata. Basi shikamana na Mwenyezi Mungu akuhifadhi na shari lao, kwani Yeye ni Mwenye kuyasikia maneno yao , ni Mwenye kuyaona matendo yao, na Atawalipa kwayo |