Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 64 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿ٱللَّهُ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ قَرَارٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡۖ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[غَافِر: 64]
﴿الله الذي جعل لكم الأرض قرارا والسماء بناء وصوركم فأحسن صوركم ورزقكم﴾ [غَافِر: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewafanyia hii ardhi ili mtulie hapo, Akawasahilishia kukaa juu yake, Akawafanyia mbingu kuwa ni sakafu ya ardhi, Akaeneza huko alama zenye kuongoza, Akawaumba kwa namna kamilifu zaidi na maumbile mazuri zaidi, Akawaneemesha kwa riziki ya halali na vilaji na vinywaji vyenye ladha. Huyo Aliyewaneemesha nyinyi neema hizi ndiye Mola wenu, Mwingi wa kheri, fadhila na baraka, na Ameepukana na kila kisichonasibiana na Yeye. Na Yeye Ndiye Mola wa viumbe wote |