Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 82 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِنۡهُمۡ وَأَشَدَّ قُوَّةٗ وَءَاثَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ ﴾
[غَافِر: 82]
﴿أفلم يسيروا في الأرض فينظروا كيف كان عاقبة الذين من قبلهم كانوا﴾ [غَافِر: 82]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawakutembea kwenye ardhi wakanushaji hawa wakafikiria juu ya maangamivu ya ummah waliokanusha waliokuwa kabla yao ulikuwa vipi mwisho wao? Ummah hao waliopita walikuwa ni wengi kuliko wao kwa idadi, zana na athari ya majengo, viwanda, ukulima na yasiyokuwa hayo. Na yote hayo waliyoyatenda hayakuwafalia kitu ilipowateremkia wao adhabu ya Mwenyezi Mungu |