Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 83 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿فَلَمَّا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَرِحُواْ بِمَا عِندَهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ ﴾
[غَافِر: 83]
﴿فلما جاءتهم رسلهم بالبينات فرحوا بما عندهم من العلم وحاق بهم ما﴾ [غَافِر: 83]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Walipowajia, hao ummah waliowakanusha, Mitume wao kwa dalili zilizo wazi, walifurahia, kwa ujinga wao, ujuzi walionao unaogongana na yale waliyokuja nayo Mitume, na ikawashukia wao ile adhabu waliokuwa wakiiharakisha kwa njia ya shere na dhihaka. Katika aya hii kuna dalili kuwa kila ujuzi unaogongana na Uislamu au kuutia kombo au kutilia shaka usahihi wake, basi ujuzi huo ni mwenye kutukanika na kuchukiza, na mwenye kuuamini si miongoni mwa wafuasi wa Muhammad, reheme ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |