Quran with Swahili translation - Surah Fussilat ayat 5 - فُصِّلَت - Page - Juz 24
﴿وَقَالُواْ قُلُوبُنَا فِيٓ أَكِنَّةٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ وَفِيٓ ءَاذَانِنَا وَقۡرٞ وَمِنۢ بَيۡنِنَا وَبَيۡنِكَ حِجَابٞ فَٱعۡمَلۡ إِنَّنَا عَٰمِلُونَ ﴾
[فُصِّلَت: 5]
﴿وقالوا قلوبنا في أكنة مما تدعونا إليه وفي آذاننا وقر ومن بيننا﴾ [فُصِّلَت: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanasema hawa wenye kukataa na kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, «Nyoyo zetu zina vifiniko venye kutuzuilia tusielewe unayotuambia, na masikizi yetu yana uziwi hatusikii, na baina yetu sisi na wewe, ewe Muhammad, pana pazia inayotuzuia kuitika mwito wako. Basi fanya kulingana na dini yako , kama ambavyo sisi tunavyofanya kulingana na dini yetu.» |