Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 44 - الشُّوري - Page - Juz 25
﴿وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن وَلِيّٖ مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَتَرَى ٱلظَّٰلِمِينَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَ يَقُولُونَ هَلۡ إِلَىٰ مَرَدّٖ مِّن سَبِيلٖ ﴾
[الشُّوري: 44]
﴿ومن يضلل الله فما له من ولي من بعده وترى الظالمين لما﴾ [الشُّوري: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na yule ambaye Mwenyezi Mungu Anampoteza na kumweka kando na uongofu kwa sababu ya udhalimu wake, hatakuwa na mtu wa kumsaidia na kumuelekeza njia ya uongofu. Na utawaona, ewe Mtume, wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, watakapo kuiona adhabu, wakisema, kumwambia Mola wao, «Je, tuna njia yoyote ya kurejea duniani ili tufanye matendo ya utiifu kwako?» Na ombi hilo halitakubaliwa kwao |