Quran with Swahili translation - Surah Az-Zukhruf ayat 11 - الزُّخرُف - Page - Juz 25
﴿وَٱلَّذِي نَزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ بِقَدَرٖ فَأَنشَرۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗاۚ كَذَٰلِكَ تُخۡرَجُونَ ﴾
[الزُّخرُف: 11]
﴿والذي نـزل من السماء ماء بقدر فأنشرنا به بلدة ميتا كذلك تخرجون﴾ [الزُّخرُف: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Aliyeteremsha kutoka mawinguni mvua kwa kipimo, Asiifanye mafuriko yenye kuzamisha wala pungufu isiyotosheleza haja, ipate kuendesha maisha yenu na yale ya wanyama wenu, tukahuisha kwa maji hayo sehemu kubwa ya ardhi kavu isiyokuwa na mimea. Na kama tulivyotoa kwa maji hayo tuliyoyateremsha kutoka juu, kwenye ardhi hiyo iliyokufa, mimea na mazao, hivo ndivyo mtakavyotolewa, enyi watu, makaburini mwenu baada ya kutoweka kwenu |