Quran with Swahili translation - Surah Az-Zukhruf ayat 32 - الزُّخرُف - Page - Juz 25
﴿أَهُمۡ يَقۡسِمُونَ رَحۡمَتَ رَبِّكَۚ نَحۡنُ قَسَمۡنَا بَيۡنَهُم مَّعِيشَتَهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَرَفَعۡنَا بَعۡضَهُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَتَّخِذَ بَعۡضُهُم بَعۡضٗا سُخۡرِيّٗاۗ وَرَحۡمَتُ رَبِّكَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ ﴾
[الزُّخرُف: 32]
﴿أهم يقسمون رحمة ربك نحن قسمنا بينهم معيشتهم في الحياة الدنيا ورفعنا﴾ [الزُّخرُف: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, wao ndio wanaougawa huu utume wakauweka wanapotaka? Sisi tumewagawia wao maisha yao katika uhai wao wa kilimwengu ya riziki na vyakula, na tumewainua daraja baadhi yao juu ya wengine : huyu ni tajiri na huyu ni masikini, huyu ana nguvu na huyu ni mnyonge, ili baadhi yao wawe ni wenye kutumiwa na wengine katika maisha. Na rehema ya Mola wako, ewe Mtume, ya kuwatia wao Peponi ni bora kuliko takataka za dunia zenye kutoweka |