Quran with Swahili translation - Surah Az-Zukhruf ayat 36 - الزُّخرُف - Page - Juz 25
﴿وَمَن يَعۡشُ عَن ذِكۡرِ ٱلرَّحۡمَٰنِ نُقَيِّضۡ لَهُۥ شَيۡطَٰنٗا فَهُوَ لَهُۥ قَرِينٞ ﴾
[الزُّخرُف: 36]
﴿ومن يعش عن ذكر الرحمن نقيض له شيطانا فهو له قرين﴾ [الزُّخرُف: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mwenye kuupa mgongo utajo wa Mwingi wa Rehema, nao ni Qur’ani, asiogope mateso yaliyotajwa ndani yake na asijiongoze kwa uongofu wake, tutamwekea Shetani hapa duniani wa kumpoteza, ikiwa ni malipo yake ya kuupa mgongo kwake utajo wa Mwenyezi Mungu. Shetani huyo atakuwa na yeye wakati wote na kufuatana naye, akimkataza ya halali na kumsukuma afanye ya haramu |