Quran with Swahili translation - Surah Ad-Dukhan ayat 59 - الدُّخان - Page - Juz 25
﴿فَٱرۡتَقِبۡ إِنَّهُم مُّرۡتَقِبُونَ ﴾
[الدُّخان: 59]
﴿فارتقب إنهم مرتقبون﴾ [الدُّخان: 59]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi ngojea, ewe Mtume, ushindi niliokuahidi juu ya hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na adhabu itakayowashukia. Wao ni wenye kungojea kufa kwako, kukushinda na kukulazimisha. Basi watajua utakuwa ni wa nani ushindi, kufaulu na sauti ya juu duniani na Akhera. Hivyo ni vyako wewe, ewe Mtume, na vya wale Waumini waliokufuata |