×

Surah Ad-Dukhaan in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah Ad Dukhaan

Translation of the Meanings of Surah Ad Dukhaan in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah Ad Dukhaan translated into Swahili, Surah Ad-Dukhaan in Swahili. We provide accurate translation of Surah Ad Dukhaan in Swahili - السواحيلية, Verses 59 - Surah Number 44 - Page 496.

بسم الله الرحمن الرحيم

حم (1)
H'a Mim
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ (2)
Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ (3)
Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji
فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ (4)
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima
أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ (5)
Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma
رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (6)
Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua
رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ (7)
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini
لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ (8)
Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo
بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ (9)
Lakini wao wanacheza katika shaka
فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ (10)
Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri
يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ (11)
Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu
رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ (12)
Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini
أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ (13)
Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha
ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ (14)
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu
إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ (15)
Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile
يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ (16)
Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa
۞ وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ (17)
Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu
أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ (18)
Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu
وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ (19)
Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi
وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ (20)
Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe
وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ (21)
Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami
فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ (22)
Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu
فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ (23)
Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa
وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ (24)
Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa
كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (25)
Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha
وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ (26)
Na mimea na vyeo vitukufu
وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ (27)
Na neema walizo kuwa wakijistareheshea
كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ (28)
Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ (29)
La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula
وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ (30)
Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha
مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ (31)
Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka
وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ (32)
Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe
وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ (33)
Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi
إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ (34)
Hakika hawa wanasema
إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ (35)
Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi
فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ (36)
Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli
أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَاهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ (37)
Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ (38)
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo
مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (39)
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ (40)
Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote
يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ (41)
Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa
إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (42)
Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu
إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ (43)
Hakika Mti wa Zaqqum
طَعَامُ الْأَثِيمِ (44)
Ni chakula cha mwenye dhambi
كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ (45)
Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
كَغَلْيِ الْحَمِيمِ (46)
Kama kutokota kwa maji ya moto
خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ (47)
(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu
ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ (48)
Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ (49)
Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ (50)
Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ (51)
Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (52)
Katika mabustani na chemchem
يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ (53)
Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ (54)
Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini
يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ (55)
Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ (56)
Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu
فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (57)
Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ (58)
Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka
فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ (59)
Ngoja tu, na wao wangoje pia
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas