Quran with Swahili translation - Surah Al-Jathiyah ayat 13 - الجاثِية - Page - Juz 25
﴿وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا مِّنۡهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ ﴾
[الجاثِية: 13]
﴿وسخر لكم ما في السموات وما في الأرض جميعا منه إن في﴾ [الجاثِية: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Akawadhalilishia kila kilichoko mbinguni miongoni mwa jua , mwezi na nyota, na kila kilicho ardhini miongoni mwa wanyama, miti, majahazi na visiokuwa hivyo kwa ajili ya maslahi yenu. Neema zote hizi ni vipaji Alizowaneemesha nazo Mwenyezi Mungu Peke Yake na fadhila inayotoka Kwake Aliyowafadhili nayo. Basi Yeye Peke Yake muabuduni, na msimfanye yoyote kuwa ni mshirika Wake. Hakika katika vitu vile Alivyowadhalilishia Mwenyezi Mungu kuna alama na dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kuzitia akilini aya za Mwenyezi Mungu, hoja Zake na dalili Zake, wakazizingatia |