Quran with Swahili translation - Surah Al-Jathiyah ayat 17 - الجاثِية - Page - Juz 25
﴿وَءَاتَيۡنَٰهُم بَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِۖ فَمَا ٱخۡتَلَفُوٓاْ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ ﴾
[الجاثِية: 17]
﴿وآتيناهم بينات من الأمر فما اختلفوا إلا من بعد ما جاءهم العلم﴾ [الجاثِية: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tukawapatia Wana wa Isrāīl Sheria zilizo wazi juu ya halali na haramu, na dalili zenye kutenganisha haki na batili. Hawakutafautiana isipokuwa baada ya kujiwa na elimu na hoja ikasimama juu yao. Na lililowapelekea wafanye hivyo ni lile jambo la kudhulumiana wao kwa wao kwa kutaka ukubwa na uongozi. Hakika Mola wako Atahukumu baina ya wanaotafautiana miongoni mwa Wana wa Isrāīl Siku ya Kiyama katika yale waliokuwa wakitafautiana juu yake duniani. Kwenye maelezo haya pana onyo kwa ummah huu wasifuate mwenendo wao |