Quran with Swahili translation - Surah Al-Jathiyah ayat 24 - الجاثِية - Page - Juz 25
﴿وَقَالُواْ مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنۡيَا نَمُوتُ وَنَحۡيَا وَمَا يُهۡلِكُنَآ إِلَّا ٱلدَّهۡرُۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِنۡ هُمۡ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴾
[الجاثِية: 24]
﴿وقالوا ما هي إلا حياتنا الدنيا نموت ونحيا وما يهلكنا إلا الدهر﴾ [الجاثِية: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanasema hawa washirikina, “Hakuna maisha isipokuwa haya maisha yetu ya duniani tuliyonayo; hakuna maisha mengineyo,” kwa njia ya kukanusha kufufuliwa baada ya kufa. “Na hakuna kinachotuangamiza isipokuwa kupitiwa na masiku na michana na umri mrefu,“ wakikanusha kuwa wana Mola Anaowatowesha na kuwaangamiza.” Na hawa washirikina hawana ujuzi wowote juu ya hilo, hawana lolote isipokuwa ni kusema kwa kudhania, kufikiria na kuwaza |