Quran with Swahili translation - Surah Al-Jathiyah ayat 31 - الجاثِية - Page - Juz 25
﴿وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَفَلَمۡ تَكُنۡ ءَايَٰتِي تُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡ وَكُنتُمۡ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ ﴾
[الجاثِية: 31]
﴿وأما الذين كفروا أفلم تكن آياتي تتلى عليكم فاستكبرتم وكنتم قوما مجرمين﴾ [الجاثِية: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ama wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, wakawakanusha Mitume Wake, na wasifuate Sheria Yake kivitendo, basi wataambiwa kwa kukaripiwa na kulaumiwa, «Kwani aya zangu hazikuwa zikisomwa kwenu huko duniani, mkazifanyia kiburi kwa kutozisikiliza na kutoziamini, na mkawa ni watu wenye kushirikisha, mnachuma maasia na hamuamini thawabu wala mateso?» |