Quran with Swahili translation - Surah Muhammad ayat 16 - مُحمد - Page - Juz 26
﴿وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُ إِلَيۡكَ حَتَّىٰٓ إِذَا خَرَجُواْ مِنۡ عِندِكَ قَالُواْ لِلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مَاذَا قَالَ ءَانِفًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡ ﴾
[مُحمد: 16]
﴿ومنهم من يستمع إليك حتى إذا خرجوا من عندك قالوا للذين أوتوا﴾ [مُحمد: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa hawa wanafiki kuna wanaokusikiliza bila ya kuelewa, kwa madharau na kupuuza, mpaka wanapoondoka kutoka kwenye kikao chako, huwa wakisema wakiwaambia wale waliohudhuria kikao chako kati ya wale wenye ujuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa njia ya shere, «Amesema nini Muhammad hivi sasa?» Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amezipiga muhuri nyoyo zao, zikawa haziielewi haki wala hawaongokei kuifikia, na wakayafuata matamanio yao katika ukafiri na upotevu |