Quran with Swahili translation - Surah Muhammad ayat 26 - مُحمد - Page - Juz 26
﴿ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لِلَّذِينَ كَرِهُواْ مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ سَنُطِيعُكُمۡ فِي بَعۡضِ ٱلۡأَمۡرِۖ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِسۡرَارَهُمۡ ﴾
[مُحمد: 26]
﴿ذلك بأنهم قالوا للذين كرهوا ما نـزل الله سنطيعكم في بعض الأمر﴾ [مُحمد: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kule kuwanyoshea wao mpaka wakolee kwenye ukafiri, ni kwa kuwa wao walisema kuwaambia Mayahudi waliokanusha Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, «Tutawatii katika baadhi ya mambo ambayo yako kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume Wake.» Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anayajua wanayoyaficha na wanayoydhihirisha. Basi Muislamu ajihadhari na kumtii asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyo kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, na amri ya Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |