Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 104 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُواْ حَسۡبُنَا مَا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَآؤُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَهۡتَدُونَ ﴾
[المَائدة: 104]
﴿وإذا قيل لهم تعالوا إلى ما أنـزل الله وإلى الرسول قالوا حسبنا﴾ [المَائدة: 104]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hawa makafiri, wanaoharamisha yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu, wanapoambiwa, «Njooni kwenye hukumu zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu na uwamuzi wa Mtume Wake, ili halali na haramu ziwafunukie, wao huwa wakisema, «Yanatutosha yale tuliyoyarithi kwa baba zetu ya maneno na vitendo.» Je wanayasema hayo ingawa baba zao walikuwa hawajui chochote: yaani, hawaielewi haki, hawaitambui wala hawaongoki kuifikia? Basi vipi watawafuata na hali ni hii? Kwa kweli, hakuna mwenye kuwafuata isipokua mjinga zaidi kuliko wao na mpotevu zaidi wa njia |