Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 15 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ كَثِيرٗا مِّمَّا كُنتُمۡ تُخۡفُونَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَعۡفُواْ عَن كَثِيرٖۚ قَدۡ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٞ وَكِتَٰبٞ مُّبِينٞ ﴾
[المَائدة: 15]
﴿ياأهل الكتاب قد جاءكم رسولنا يبين لكم كثيرا مما كنتم تخفون من﴾ [المَائدة: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi watu mliopewa Kitabu , miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara! Amewajia nyinyi mjumbe wetu Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwafafanulia mengi ambayo mlikuwa mkiyaficha kwa watu katika yale yaliyomo ndani ya Taurati na Injili, na kuacha kuyafafanua yale ambayo busara haitaki yafafanuliwe. Hakika umewajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwngaza na Kitabu chenye ufafanuzi, nacho ni Qur’ani tukufu |