Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 23 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمَا ٱدۡخُلُواْ عَلَيۡهِمُ ٱلۡبَابَ فَإِذَا دَخَلۡتُمُوهُ فَإِنَّكُمۡ غَٰلِبُونَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ﴾
[المَائدة: 23]
﴿قال رجلان من الذين يخافون أنعم الله عليهما ادخلوا عليهم الباب فإذا﴾ [المَائدة: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Walisema watu wawili kati ya wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ambao Mwenyezi Mungu Aliwapa neema kwa kumtii kwao Yeye na kumtii Mtume Wake, kuwaambia Wana wa Isrāīl, «Ingieni kwa majabari hao kupitia lango la mji wao, ikiwa ni mojawapo ya njia za kutafuta sababu za ushindi. Mtakapoingia langoni, mtawashinda. Na kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, jitegemezeni, iwapo nyinyi mnamuamini Mtume Wake katika yale Aliyowaletea, mnaiandama sheria Yake kivitendo.» |