×

Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake 5:33 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:33) ayat 33 in Swahili

5:33 Surah Al-Ma’idah ayat 33 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 33 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿إِنَّمَا جَزَٰٓؤُاْ ٱلَّذِينَ يُحَارِبُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوٓاْ أَوۡ يُصَلَّبُوٓاْ أَوۡ تُقَطَّعَ أَيۡدِيهِمۡ وَأَرۡجُلُهُم مِّنۡ خِلَٰفٍ أَوۡ يُنفَوۡاْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِۚ ذَٰلِكَ لَهُمۡ خِزۡيٞ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴾
[المَائدة: 33]

Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إنما جزاء الذين يحاربون الله ورسوله ويسعون في الأرض فسادا أن يقتلوا, باللغة السواحيلية

﴿إنما جزاء الذين يحاربون الله ورسوله ويسعون في الأرض فسادا أن يقتلوا﴾ [المَائدة: 33]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na wanaojitokeza wazi kumfanyia uadui na kuzifanyia uadui hukumu zake na hukumu za Mtume Wake na kufanya uharibifu katika ardhi kwa kuwaua watu na kupora mali, ni wauawe au wasulubiwe pamoja na kuuawa (Kusululubiwa ni kufungwa mhalifu juu ya bao) au ukatwe mkono wa kulia wa mpiga vita na mguu wake wa kushoto. Iwapo hatatubu {kwa kuendelea na uharamia wake}, ukatwe mkono wake wa kushoto na mguu wa kulia, au wahamishwe wapelekwe mji usiokuwa wao, wafungwe kwenye jela ya mji huo mpaka iyonekane toba yao. Na haya ndiyo malipo Aliyoyaandika Mwenyezi Mungu kwa wenye kupiga vita; nayo ni unyonge wa duniani. Na huko Akhera itawapata adhabu kali iwapo hawatatubia
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek