Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 72 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿لَقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمۡۖ إِنَّهُۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَىٰهُ ٱلنَّارُۖ وَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ ﴾
[المَائدة: 72]
﴿لقد كفر الذين قالوا إن الله هو المسيح ابن مريم وقال المسيح﴾ [المَائدة: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaapa kwamba wale ambao walisema, «Mwenyezi Mungu Ndiye al-Masīh, mwana wa Maryam,» wameshakufuru kwa maneno yao haya. Na Alitoa habari Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwamba al- Masīh, alisema kuwaambia Wana wa Isrāīl, «Muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika, kwani mimi na nyinyi katika uja tuko sawa.» Kwa hakika, yoyote atakayemuabudu mwengine, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliye Pweke, basi Mwenyezi Mungu Ataifanya Pepo kuwa ni haramu kwake na Ataufanya Moto kuwa ndio makao yake na hatakuwa na msaidizi wa kumuokoa nao Moto huo |