Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 73 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ ثَالِثُ ثَلَٰثَةٖۘ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّآ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ وَإِن لَّمۡ يَنتَهُواْ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴾
[المَائدة: 73]
﴿لقد كفر الذين قالوا إن الله ثالث ثلاثة وما من إله إلا﴾ [المَائدة: 73]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wamekufuru Wanaswara waliosema, «Mwenyezi Mungu ni mkusanyiko wa vitu vitatu: Baba, Mwana na Roho mtakatifu.» Kwani Wanaswara hawa hawakujua kwamba watu hawana isipokuwa muabudiwa Mmoja, Hakuzaa wala Hakuzaliwa? Na iwapo wenye kusema maneno haya hawatakoma na uzushi wao na urongo wao, hakika itawapata wao adhabu iliyo kali iumizayo kwa sababu ya kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu |