Quran with Swahili translation - Surah Al-hashr ayat 14 - الحَشر - Page - Juz 28
﴿لَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرٗى مُّحَصَّنَةٍ أَوۡ مِن وَرَآءِ جُدُرِۭۚ بَأۡسُهُم بَيۡنَهُمۡ شَدِيدٞۚ تَحۡسَبُهُمۡ جَمِيعٗا وَقُلُوبُهُمۡ شَتَّىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡقِلُونَ ﴾
[الحَشر: 14]
﴿لا يقاتلونكم جميعا إلا في قرى محصنة أو من وراء جدر بأسهم﴾ [الحَشر: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hawatakabiliana na nyinyi Mayahudi wakiwa wamejikusanya isipokuwa wakiwa kwenye miji iliyohifadhiwa kwa ngome na mahandaki, au nyuma ya kuta ambazo wanazitumia kwa kujificha kwa uoga wao na kicho kilichojikita ndani ya nyoyo zao. Uadui wao baina yao ni mkubwa, utadhani kuwa wao wamekusanyika kwenye neno moja, lakini nyoyo zao ziko mbalimbali, na hiyo ni kwa sababu wao ni watu wasioitia akilini amri ya Mwenyezi Mungu wala kuzizingatia aya Zake |