Quran with Swahili translation - Surah Al-hashr ayat 24 - الحَشر - Page - Juz 28
﴿هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡخَٰلِقُ ٱلۡبَارِئُ ٱلۡمُصَوِّرُۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ﴾
[الحَشر: 24]
﴿هو الله الخالق البارئ المصور له الأسماء الحسنى يسبح له ما في﴾ [الحَشر: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, kutakasika ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Aliye Muumba, Muanzilishi wa uumbaji kulingana na hekima Yake, Aliyewapa sura viumbe Wake kwa namna Atakavyo. Ni Yake Yeye, kutakasika ni Kwake, Majina Mema na sifa tukufu. Vinamatakasa Yeye vyote vilivyoko mbinguni na ardhini, na Yeye ni Mshindi, Mkali wa mateso kwa maadui Wake, Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo ya viumbe Vyake |