×

Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa walio 6:124 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:124) ayat 124 in Swahili

6:124 Surah Al-An‘am ayat 124 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 124 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿وَإِذَا جَآءَتۡهُمۡ ءَايَةٞ قَالُواْ لَن نُّؤۡمِنَ حَتَّىٰ نُؤۡتَىٰ مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ رُسُلُ ٱللَّهِۘ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ حَيۡثُ يَجۡعَلُ رِسَالَتَهُۥۗ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ صَغَارٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعَذَابٞ شَدِيدُۢ بِمَا كَانُواْ يَمۡكُرُونَ ﴾
[الأنعَام: 124]

Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa walio pewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإذا جاءتهم آية قالوا لن نؤمن حتى نؤتى مثل ما أوتي رسل, باللغة السواحيلية

﴿وإذا جاءتهم آية قالوا لن نؤمن حتى نؤتى مثل ما أوتي رسل﴾ [الأنعَام: 124]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na pindi inapowajia washirikina hawa, miongoni mwa watu wa Maka, hoja iliyo waziwazi juu ya unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wanasema baadhi ya wakubwa wao, «Kamwe hatutaukubali unabii wake mpaka Mwenyezi Mungu Atupe unabii na miujiza mfano wa Aliyowapa wajumbe wake waliotangulia» Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliwajibu kwa neno lake,: “Mwenyezi Mungu Anajua zaidi wapi Auweke ujumbe Wake.» Kwa maana kuwa Anawajua wale wanaofaa kubeba ujumbe Wake na kuufikisha kwa Watu. Utawapata unyonge wakiukaji mipaka hawa, na watakuwa na adhabu iumizayo ndani ya Moto wa Jahanamu kwa sababu ya vitimbi vyao kwa Uislamu na watu wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek