Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 125 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهۡدِيَهُۥ يَشۡرَحۡ صَدۡرَهُۥ لِلۡإِسۡلَٰمِۖ وَمَن يُرِدۡ أَن يُضِلَّهُۥ يَجۡعَلۡ صَدۡرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجٗا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي ٱلسَّمَآءِۚ كَذَٰلِكَ يَجۡعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الأنعَام: 125]
﴿فمن يرد الله أن يهديه يشرح صدره للإسلام ومن يرد أن يضله﴾ [الأنعَام: 125]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumuafukia aikubali haki, Anakikunjua kifua chake kukubali Imani na upweke wa Mwenyezi Mungu; na yule ambaye Anataka kumpoteza , Anakifanya kifua chake kiwe katika hali ya dhiki kubwa na kukunjika katika kuukubali uongofu, kama hali ya anayepaa kwenye tabaka za anga za juu, hapo akapatwa na uzito mkubwa wa kuvuta pumzi. Na kama anavyovifanya Mwenyezi Mungu vifua vya makafiri vibanike sana na kukunjika, hivyo basi ndivyo Atakavyowapatia adhabu wale wasiomuamini |