Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 130 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي وَيُنذِرُونَكُمۡ لِقَآءَ يَوۡمِكُمۡ هَٰذَاۚ قَالُواْ شَهِدۡنَا عَلَىٰٓ أَنفُسِنَاۖ وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ ﴾
[الأنعَام: 130]
﴿يامعشر الجن والإنس ألم يأتكم رسل منكم يقصون عليكم آياتي وينذرونكم لقاء﴾ [الأنعَام: 130]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi majini na binadamu mlio washirikina, kwani hawakuwajia Mitume miongoni mwenu- Maandiko yanaonesha kuwa Mitume wanatoka kwa wanadamu tu.- wanaowapa habari za alama zangu zilizo wazi, zinazokusanya maamrisho na makatazo, zinazofafanua kheri na shari na wanaowaonya kukumbana na adhabu yangu Siku ya Kiyama? Watasema washirikina hawa, maijini na binadamu, «Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu kwamba Mitume wako wametufikishia aya zako na wametuonya makutano ya Siku yetu hii, na sisi tukawakanusha.» Na hawa washirikina, liliwadanganya wao pambo la maisha ya dunia. Na walizishuhudilia nafsi zao kwamba wao walikuwa wakiukataa upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na wakiwafanya warongo Mitume Wake, amani iwashukie |