Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 135 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿قُلۡ يَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَامِلٞۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُۥ عَٰقِبَةُ ٱلدَّارِۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ ﴾
[الأنعَام: 135]
﴿قل ياقوم اعملوا على مكانتكم إني عامل فسوف تعلمون من تكون له﴾ [الأنعَام: 135]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, «Enyi watu wangu, fanyeni kwa njia yenu, na mimi nitafanya kwa njia yangu ambayo Mola wangu, Aliyetukuka na kuwa juu, Aliniwekea. Mtakuja kujua, pindi mateso yatakapowashukia, ni nani atakayekuwa na mwisho mwema?» Hakika hatafaulu kupata radhi za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na Pepo yule aliyekiuka mpaka Wake na akadhulumu, na akamshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu asiyekuwa Yeye |