Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 27 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَى ٱلنَّارِ فَقَالُواْ يَٰلَيۡتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[الأنعَام: 27]
﴿ولو ترى إذ وقفوا على النار فقالوا ياليتنا نرد ولا نكذب بآيات﴾ [الأنعَام: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau utawaona, ewe Mtume, washirikina hawa Siku ya Kiyama, utaona jambo kubwa, nalo ni wakati wao watakapofungwa juu ya Moto, na watakaposhuhudia yaliyomo humo miongoni mwa minyororo na pingu, na kujionea kwa macho yao mambo makubwa hayo na vituko hivyo. Hapo watasema, «Twatamani turudishwe kwenye maisha ya kilimwengu, tupate kuziamini aya za Mwenyezi Mungu na tuzitumie na tuwe ni miongoni mwa Waumini.» |