×

Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na 6:34 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:34) ayat 34 in Swahili

6:34 Surah Al-An‘am ayat 34 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 34 - الأنعَام - Page - Juz 7

﴿وَلَقَدۡ كُذِّبَتۡ رُسُلٞ مِّن قَبۡلِكَ فَصَبَرُواْ عَلَىٰ مَا كُذِّبُواْ وَأُوذُواْ حَتَّىٰٓ أَتَىٰهُمۡ نَصۡرُنَاۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ وَلَقَدۡ جَآءَكَ مِن نَّبَإِيْ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ﴾
[الأنعَام: 34]

Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu. Na hapana wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na bila ya shaka zimekujia baadhi ya khabari za Mitume hao

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولقد كذبت رسل من قبلك فصبروا على ما كذبوا وأوذوا حتى أتاهم, باللغة السواحيلية

﴿ولقد كذبت رسل من قبلك فصبروا على ما كذبوا وأوذوا حتى أتاهم﴾ [الأنعَام: 34]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika makafiri waliwakanusha Mitume kabla yako Aliyowatuma Mwenyezi Mungu, Aliyotukuka, kwa umma wao. Wao waliudhiwa katika kufuata njia Yake na wakasubiri juu ya hilo na wakaendelea katika ulinganizi wao na bidii yao mpaka ikawajia nusura ya Mwenyezi Mungu. Na hakuna mwenye kuyageuza maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni yale Aliyoyateremsha kwa Nabii Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yenye ahadi Yake kwamba Atampa ushindi juu ya wanaomfanyia uadui. Na hakika imekujia wewe, ewe Mtume, habari ya Mitume waliokuwa kabla yako na nusura ya Mwenyezi Mungu iliyohakikishika kwao na mateso ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu Zake zilizowafikia wenye kuwakanausha. Basi wewe una kiolezo chema na mfano wa kuiga kutoka kwa Mitume waliotangulia. Katika hili pana kumliwaza Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek