Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 56 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿قُلۡ إِنِّي نُهِيتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۚ قُل لَّآ أَتَّبِعُ أَهۡوَآءَكُمۡ قَدۡ ضَلَلۡتُ إِذٗا وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُهۡتَدِينَ ﴾
[الأنعَام: 56]
﴿قل إني نهيت أن أعبد الذين تدعون من دون الله قل لا﴾ [الأنعَام: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, Amenikataza niabudu masanamu ambao mnaowaabudu badala Yake.» Na uwaambie, «Sitafuata matamanio yenu. Nitakuwa nimepotea njia ya sawa nikifuata matamanio yenu na sitakuwa ni miongoni mwa walioongoka.» |