Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 57 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿قُلۡ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبۡتُم بِهِۦۚ مَا عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦٓۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ يَقُصُّ ٱلۡحَقَّۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰصِلِينَ ﴾
[الأنعَام: 57]
﴿قل إني على بينة من ربي وكذبتم به ما عندي ما تستعجلون﴾ [الأنعَام: 57]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mimi niko kwenye hoja iliyo wazi ya sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyoniletea kwa njia ya wahyi. Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa ibada. Na hili mlilikanusha. Na haliko kwenye uwezo wangu jambo la kuwateremshia adhabu mnayoitaka kwa haraka. Na uamuzi wa kuchelewesha hilo uko tu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Yeye Anahadithia ukweli na Yeye Ndiye bora wa kupambanua baina ya haki na batili kwa uamuzi Wake na hukumu Yake.» |