Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 81 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَكَيۡفَ أَخَافُ مَآ أَشۡرَكۡتُمۡ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمۡ أَشۡرَكۡتُم بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنٗاۚ فَأَيُّ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ أَحَقُّ بِٱلۡأَمۡنِۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴾
[الأنعَام: 81]
﴿وكيف أخاف ما أشركتم ولا تخافون أنكم أشركتم بالله ما لم ينـزل﴾ [الأنعَام: 81]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na ni vipi nitaogopa masanamu yenu na hali nyinyi hamumuogopi Mola wangu Aliyewaumba na Akayaumba masanamu yenu ambayo mnamshirikisha nayo Mwenyezi Mungu katika ibada, bila ya kuwa na hoja yoyote juu ya hilo? Basi ni lipi kati ya makundi mawili, kundi la washirikina na kundi la wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, lenye haki zaidi ya utulivu na usalama na kuaminika na adhabu ya Mwenyezi Mungu? Iwapo mnajua ukweli wa ninayoyasema, niambieni.» |