Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 9 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ مَلَكٗا لَّجَعَلۡنَٰهُ رَجُلٗا وَلَلَبَسۡنَا عَلَيۡهِم مَّا يَلۡبِسُونَ ﴾
[الأنعَام: 9]
﴿ولو جعلناه ملكا لجعلناه رجلا وللبسنا عليهم ما يلبسون﴾ [الأنعَام: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau kama tulimfanya mtume aliyeteremshwa kwao ni Malaika, kwani hawakukinai na Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, tungalimfanya Malaika huyo kwenye sura za mwanadamu, ili waweze kumsikia na kusema naye. Kwani haimkiniki kwao kumuona Malaika katika sura zake za kimalaika. Na lau Malaika aliwajia kwa sura za mtu, jambo hilo lingaliwafanya wachanganyikiwe kama lilivyowafanya wachanganyikiwe jambo la Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |